Sunday, March 22, 2015

Mkuu wa Wila ya Moshi, Novatus Makunga(kushoto) akimkabidhi kikombe mchoma nyama mkuu wa Bar Kill Home ya Moshi mjini, Said Gora  mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya Safari Nyama Choma mkoani Kilimanjaro yaliyofanyika katika Uwanja wa Hugos zamani Pan African mwishoni mwa wiki.Katikati ni Meneja wa bia ya Safari Lger, Edith Bebwa.
Mashabiki wa Bar ya Kill Home ya Moshi mjini wakishangilia kwa kucheza  mara baada ya kutangazwa mabingwa katika mashindano ya Safari Lager Nyama Choma mkoani humo yaliyofanyika katika Uwanja wa Hogos zamani Pan African mwishoni mwa wiki.Bingwa alizawadiwa Kikombe na pesa taslimu Shilingi 1,000 000/=.
Na Mwandishi Wetu.Moshi-Kilimanjaro.
KILL Home Bar Moshi mkoani Kilimanjaro wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2015 yaliyofanyiaka mswishoni mwa wiki katika Uwanja wa Hugos zama ni Pan Africa  na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja na Kikombe.
Nafasi ya pili ilichukuliwa Rau Bar ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 800,000/=,nafasi ya tatu ni Makanyaga  Bar ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/=,nafasi ya nne ni Lamina Bar ambayo ilizawadiwa Shilingi 400,000/= na nafasi ya tano ni White Star Bar ambayo ilizawadiwa Shingi 200,000/-
Akizungumza na wakazi Moshi na vijitongoji jirani walifika katika mashindano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga, kwanza aliwashukuru kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kwa kuendea kudhamini mashindano ya Nyama Choma ambapo kwa mwaka huu ni mara ya nane mfululizo kwani yamekuwa yenye mvuto wa pekee ambayo yanawapa picha halisi wakazi wa Kilimanjaro kuwa wapi wanaweza kupata nyama choma bora kutoka katika baa tano ambazo zimeingia fainali katika mkoa wetu.
Alisema Makunga kwanza kabisa tunawapongeza kwa kutoa elimu kwa wapishi wa baa mbalimbali  ambayo mliaanza nayo hapo awali tunaamini kwa kupitia  hilo wapishi wetu wameelimika si kama mlivyowakuta na hilo tunawashukuru na tunawaomba muendelee nalo kwani mnaongeza ajira kwa jamii kama si kupunguza umasikini.
Pili aliwapongeza baa tano zilizoingia fainali kwani wao ndio baa bora katika baa zote zinazochoma nyama mkoani humo na aliwaomba waendelee kuilinda hadhi na sifa hiyo waliyopewa  na mwisho aliwapongeza mabingwa wapya Kill Home Bar  kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2015 na kuwaomba ambao hawakufanikiwa kupata nafasi hiyo wajiandae kwa mashndano yajayo ya Safari Nyama Choma 2016.
Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa aliwapongeza mabingwa wa mwaka 2015,Kill Home  Bar na pia aliwashukuru wote walioshiriki toka mchakato ulipoanza mpaka kufikia kumpata bingwa lakini pia aliwashukuru wakazi wa Kilimanjaro waliojitokeza kwa wingi kuja kushuhudia nani anatwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma 2015.
Mwisho Edith aliwaomba washiriki wote ambao waliopata zawadi wakatumie vyema zawadi walizopata kwa kuboresha majiko yao kwa mashindano yajayo ya 2016 lakini pia wakawe mabalozi wazuri wa bia ya Safari Lager kwenye biashara zao.

0 comments:

Post a Comment