Monday, March 30, 2015

Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kilwa Road jijini Dar es Salaam, Lucas Mgaya(wa pili kushoto) akimkabidhi kikombe mchoma nyama mkuu wa Bar Chamanzi, Shaban Seif  mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya Safari Nyama Choma kitongoji cha Dar One Temeke Dar es Salaam yaliyofanyika katika Uwanja TCC Chang’ombe mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Meneja wa bia ya Safari Lger, Edith Bebwa.


Na Mwandishi Wetu.
KILWA ROAD Bar Dar One Temeke jijini Dar es Saalaam  wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2015 yaliyofanyiaka mwishoni mwa wiki katika viwanja vya TCC Chang’ombe  na hivyo kuzawadiwa Kikombe pamoja na nafasi ya kushiriki fainali za Mkoa  zinazotarajiwa kufanyika Aprili 12,2015 katika viwanja vya Leaders.
Nafasi ya pili ilichukuliwa Liquid Bar ambayo  kwa nafasi hiyo ilipata nafasi ya kushiriki fainali za Mkoa Leader na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Chamanzi Bar ambao pia walipata nafasi ya kushiriki fainali za Mkoa pale Leaders.
 Akizungumza na wakazi  Temeke pamoja vitongoji jirani walifika katika mashindano hayo, Mkuu wa Kituo cha Kilwa Road Polisi, Lucas Mgaya, kwanza aliwashukuru kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kwa kuendea kudhamini mashindano ya Nyama Choma ambapo kwa mwaka huu ni mara ya nane mfululizo kwani yamekuwa yenye mvuto wa pekee ambayo yanawapa picha halisi wakazi wa Temeke kuwa wapi wanaweza kupata nyama choma bora kutoka katika baa tano ambazo zimeingia fainali katika kitongoji cha Dar One.
Alisema Mgaya kwanza kabisa tunawapongeza kwa kutoa elimu kwa wapishi wa baa mbalimbali  ambayo mliaanza nayo hapo awali tunaamini kwa kupitia  hilo wapishi wetu wameelimika si kama mlivyowakuta na hilo tunawashukuru na tunawaomba muendelee nalo kwani mnaongeza ajira kwa jamii kama si kupunguza umasikini.
Pili aliwapongeza baa zilizoingia fainali kwani wao ndio baa bora katika baa zote zinazochoma nyama na aliwaomba waendelee kuilinda hadhi na sifa hiyo waliyopewa  na mwisho aliwapongeza mabingwa Kilwa Road Bar  kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2015 na kuwaomba ambao hawakufanikiwa kupata nafasi hiyo wajiandae kwa mashindano yajayo ya Safari Nyama Choma 2016.
Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa aliwapongeza mabingwa wa mwaka 2015,Kilwa Road Bar Bar na pia aliwashukuru wote walioshiriki toka mchakato ulipoanza mpaka kufikia kumpata bingwa lakini pia aliwashukuru wakazi wa Dar One Temeke waliojitokeza kwa wingi kuja kushuhudia nani anatwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma 2015.
Mwisho Edith aliwaomba washiriki wakajiandae vyema kwa mashindano ya Mkoa yanayotarajiwa kufanyika Aprili 12 pali viwanja vya Leaders.

0 comments:

Post a Comment