Wednesday, March 25, 2015

 Director, Tony Elumelu Entrepreneurship Programme (TEEP), Parminder Vir; Founder, Tony Elumelu Foundation, Tony O. Elumelu; CEO, Tony Elumelu Foundation, Reid Whitlock; and CEO and Founder of Java Foods, Zambia and Member Selection Committee TEEP, Monica Musonda during the official announcement of the selection of the first 1,000 African entrepreneurs for the Tony Elumelu Entrepreneurship Programme (TEEP) in Lagos yesterday.
CEO, Spotone Global Solution, Senegal and Member, Selection Committee, Tony Elumelu Entrepreneurship Programme (TEEP), Mariéme Jamme; Director, TEEP, Parminder Vir; Founder, Tony Elumelu Foundation, Tony O. Elumelu; CEO, Tony Elumelu Foundation, Reid Whitlock; CEO and Founder of Java Foods, Zambia and Member, Selection Committee, TEEP, Monica Musonda; Founder and Chair of Believe in Africa, Cameroon and Member, Selection Committee, Angelle Kwemo during the official announcement of the selection of the first 1,000 African entrepreneurs for the Tony Elumelu  Entrepreneurship Programme (TEEP) in Lagos yesterday. MFUKO wa Tony Elumelu (TEF) wenye makao makuu yake hapa leo umetangaza orodha ya majina ya wajasiliamali 1,000 toka nchi 52 za Afrika walioshinda shindano maalumu la kuandika wazo la kukuza biashara au kuanzisha biashara lililozinduliwa Januari 1 mwaka huu.

Jumla ya washiriki 20,000 toka nchi 52 za kiafrika walishiriki shindano hilo ambao waliwakilisha ubunifu na hazina iliyopo katika bara la Afrika. Kwa kuanza, jumla ya washindi 1,000 wamechaguliwa kwa mwaka huu wa kwanza na washindi wote wameonyesha uwezo wa kijasiliamali wa Kiafrika ambao utachochea ukuaji wa uchumi na maendeleo kwa jumla.

Akiongea manufaa ya mpango huo, Mwanzilishi wa Mfuko huo Bw Tony O. Elumelu, CON alisema: “Uchaguzi wa wajasiliamali 1000 unatusogeza katika kufanikisha lengo letu la kuchochea mageuzi ya uchumi na kijamii pamoja na kuongeza ajira barani Afrika. Japokuwa sijakutana wala kuongea na mshindi yeyote, nina uhakika kwamba kutokana na vigezo, washindi wote ni tumaini la Afrika ya baadaye. Nitandelea kuwekeza uzoefu wangu, muda, ushawishi na rasilimali ili kupata mafanikio. Nimeamua kuanza hii safari na hawa wajasiliamali nikiwa na matumanini na mavuto.”


Washindi hao wanawakilisha nchi 52 za Afrika na mipaka yake yote, ikiwemo sekta za kilimo, elimu, mitindo na Tehama. Nchi tano za kwanza kuwa na washindi wengi ni Nigeria, Kenya, Uganda, Afrika Kusini na Ghana. Kanda zote tano za Mashariki, Kusini, Kaskazini na Magharibi ziliwakilishwa, zikiwemo kanda za waafrika wanaoongea lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu. Zaidi ya hapo, wanatengeneza nafasi na ahadi kwa bara la Afrika.

Mfuko wa Tony Elumelu uliichagua kampuni ya Accenture kama mhakiki huru wa kila kazi iliyoshiriki kwa kuzingatia masharti na vigezo vilivyowekwa na kamati ya uchaguzi ya mpango huo. Uhakiki huru na mkutano wa kamati ya shindano hilo ulioshirikisha wajasiliamali na wataalamu wa maendeleo toka barani Afrika hatimaye leo umetangaza washindi 1,000 wa shindano hilo.


Washindi 1000 waliotangazwa wataendelea na mafunzo mbalimbali kwa muda wa miezi tisa. Mafunzo hayo ni pamoja na mafunzo kwa njia ya mtandao, mafunzo toka kwa wajasiliamali waliofanikiwa na kambi za mafunzo.

Zaidi ya washiriki 19,000 ambao hawakufanikiwa kwenye mchujo wa mwaka huu wataalikwa kuingia katika mtandao wa wajasiliali wa Elumelu ambapo watajifunza mbinu mbalimbali za kufanya biashara.


ParminderVir OBE, Mkurugenzi wa Ujasiliamali kwenye Mfuko wa Tony Elumelu alisema: “Ushiriki mkubwa na wenye kiwango cha hali ya juu tulioupokea ni ishara kuna vipaji ambavyo vipo hapa Afrika. Mpango wa Ujasiamali wa Tony Elumelu (TEEF) utatoa msaada  kwa hawa wajasiliamali kujikuza wenyewe pamoja na kuendeleza biashara zao. Kupitia mpango huu, manufaa ya muda mrefu ya uwekezaji na kuzaliwa kwa kizazi kipya cha ubepari wa kiafrika vinaweza kuenea bara zima la Afrika.”

Orodha ya majina ya washindi yanapatikana kwenye www.tonyelumelufoundation.org/teep

0 comments:

Post a Comment