Thursday, March 12, 2015


Barcelona, Hispania; Ijumaa, March 03 2015.

Kizazi cha tano cha teknolojia ya simu za mkononi (5G) kinategemewa kuwa nguzo muhimu sana ya miundo mbinu katika ulimwengu ujao wa teknolojia. Hayo yamesemwa na Bwana Ken Hu, Makamu mwenyekiti wa Kampuni ya Huawei ambaye kwa kupokezana yeye ndiye Mkurugenzi Mtendaji kwa sasa.

Akizungumza katika Mkutano wa Dunia wa masuala ya simu (MWC) uliofanyika jijini Barcelona nchini Hispania mwishoni mwa wiki iliyopita, Mr, Hu alisisitiza kwamba maono ya kuwa na teknolojia ya 5G yatafanikiwa kupitia ushirikiano wa sekta mbalimbali, ubunifu makini katika teknolojia na mageuzi katika mikakati ya kibiashara.

“Msukumo mkubwa wa kuwa na teknolojia ya 5G unahusisha mahitaji ya kumwezesha mtumiaji kupata urahisi kutumia, uwezekano wa vifaa vingi zaidi kutumia Internet katika maisha ya kila siku, na mahitaji ya kuwa na watoa huduma wanaozingatia sekta maalum pekee katika mapinduzi ya viwanda siku zijazo” Alisema Bwana Hu.

Aliendelea kusisitiza kwamba, “Mitandao inayotumia teknolojia ya 5G ikitumika ipasavyo inaweza kufikia zaidi ya vifaa vya kielektroniki bilioni 100 duniani kote. Uwezo huu ni muhimu sana katika teknolojia”. Bwana Hu alieleza kitaalamu kwamba, teknolojia ya 5G ina uwezo wa kufanya kazi na kutoa majibu sahihi kwa haraka sana (One-Millisecond latency), hili litarahisisha utengenezaji wa magari yanayojiendesha yenyewe, na matumizi ya viwandani ambayo huhitaji teknolojia inayofanya kazi kwa haraka sana.

Teknolojia ya 5G inategemewa kuwa na kasi ya juu sana ya kuhamisha data (10 Gbit/s), hii itafanya kuhamisha sinema ya ukubwa wa 8G HD kuchukua muda mfupi sana. Sinema ya ukubwa huu inaweza kuhamishwa kwa muda wa zaidi ya saa moja kwa kutumia teknolojia ya 3G, au inatumia dakika saba kwa teknolojia ya 4G lakini kwa kutumia teknolojia ya 5G itatumia sekunde saba tu. “Zaidi ya kuwa imeboreshwa, teknolojia ya 5G itawezesha uwepo wa miundo tofauti ya biashara na labda hata uwepo wa viwanda vipya”. Alisema Bwana Hu.


Bwana Hu aliendelea kusema, ili kufanikisha uwepo wa teknolojia ya 5G watoa huduma wanapaswa kwanza kushirikiana na kuruhusu mahitaji ya biashara kuleta maendeleo katika viwango, na ubunifu katika teknolojia. Baada ya hapo sekta hii itahitaji ubunifu makini sana katika teknolojia, mfano wa ubunifu ni uvumbuzi wa Huawei hivi karibuni unaoelekea kufanikisha teknolojia ya 5G.

Baada ya miaka mingi ya utafiti wa kiteknolojia, Huawei imefanikiwa kuendeleza teknolojia ya SCMA na F-OFDM ambazo zinaruhusu ufanyaji kazi kwa haraka zaidi. Bwana Hu alisisitiza kwamba sekta ya teknolojia inapaswa kutafiti na kuboresha maeneo mengine pia hasa usanifu wa mitandao (Network Architecture).

Mwisho kabisa, Bwana Hu alisema “Tunaamini kwamba mikakati ya namna hii itasaidia watoa huduma za simu kupata faida zaidi katika teknolojia ya 4G, itachochea uhitaji wa teknolojia ya 5G na pia itafanya waendelee kuwa vinara katika maendeleo ya teknolojia kutoka 4G kwenda 5G.

Kampuni ya Huawei mwishoni mwa mwezi February ilitangaza rasmi majaribio ya teknolojia ya 4.5G katika biashara. Ilisema kwamba teknolojia ya 4.5G ambayo itakuwa tayari kwa matumizi mwaka 2016, itaweka kidogo ubunifu ulio katika 5G uwe katika 4G iliyopo sasa. Eknolojia ya 4.5G itasaidia watoa huduma za simu kuongeza mapato kwa kutoa huduma ambazo ni bora zaidi kama kuunganisha simu nyingi zaidi, kufanya kazi kwa haraka zaidi (low latency) n.k  huduma ambazo ni bora zaidi kuliko ilivyo teknolojia ya 4G sasa hivi.

###

About Huawei
Huawei is a leading global information and communications technology (ICT) solutions provider. Our aim is to build a better connected world, acting as a responsible corporate citizen, innovative enabler for the information society, and collaborative contributor to the industry. Driven by customer-centric innovation and open partnerships, Huawei has established an end-to-end ICT solutions portfolio that gives customers competitive advantages in telecom and enterprise networks, devices and cloud computing. Huawei’s 170,000 employees worldwide are committed to creating maximum value for telecom operators, enterprises and consumers. Our innovative ICT solutions, products and services are used in more than 170 countries and regions, serving over one-third of the world's population. Founded in 1987, Huawei is a private company fully owned by its employees.

For more information, please visit Huawei online at www.huawei.com or follow us on:


0 comments:

Post a Comment