Wednesday, March 25, 2015


KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza bar tano zilizofanikiwa kuingia fainali kwenye kinyang’anyiro cha shindano la uchomaji nyama Dar  One  lijulikanalo kama “Safari Lager Nyama Choma Competition 2015”.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja mauzo Tbl kwa ukanda wa Temeke, Patrick Swai  alizitaja bar zilizoifanikiwa kuingia fainali kuwa ni;
1.Kilwa road Bar.
2.Liquid Bar.
3.Chamanzi Bar.
4.Kwetu Pazuri Bar.
5.Minazini Bar.

Alisema Swai fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma mwaka huu wa 2015 zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja TCC Chang’ombe mkoani Dar es Salaam kwa kitongoji cha Dar One kama unavyojua kwa mkoa huu wa Dar es Salaam tumeigawa katika sehemu mbili, Dar One na Dar two, hivyo tunanza na Dar One jumapili  hii ya tarehe 29 Machi 2015 katika viwanja vya TCC Chang’ombe  kuanzia saa mbili asubuhi na kuendelea tukisindikizwa Bendi ya Msondo “Baba ya Muziki”  pamoja na  DJ mkali kutoka hapahapa jijini Dar es Salaam na burudani zingine nyingi pamoja na zawadi kemkem kutoka Safari Lager..

Shindano  hili hufanyika kila mwaka, na  kwa mwaka huu linafanyika kwa  mara ya nane mfululizo na mwaka huu mkoa wetu tumekuwa wamwisho kuyafanya mashindano haya ambayo yalizinduliwa rasmi Mkoani Mbeya wiki nnei zilizopita yakafuatiwa na Mwanza, Arusha na Kilimanjaro na sasa ni Dar es Salaam.

Tangu lilipoanzishwa mwaka 2008, shindano hili limekuwa na mvuto wa kipekee kwa wanywaji wa bia ya Safari Lager kwani wamejitokeza kwa wingi kupigia kura baa zao kuhakikisha zinaibuka na ushindi katika mkoa waliopo.

Kwa mwaka huu mchakato wa kuzipata bar zilizoingia fainali ilikuwa ni wa kuipigia kura bar unayoipenda wewe mlaji wa nyama choma kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kutumia simu za mkononi kwenda namba 0653-215151. Ujumbe ambao ulitozwa gharama ya kawaida za kutuma ujumbe.

Alisema Swai “Lengo kuu la shindano la Safari Lager Nyama Choma ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora vya uchomaji na utayarishaji wa nyama choma. Tunahakikisha wachoma nyama katika baa za mikoa yote inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa kutosha katika fani hii ili kumpa mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama choma.

Tumezingatia maombi ya washiriki mwaka jana hivyo basi mwaka huu semina inayoelekeza namna nzuri ya uchomaji nyama itafanyika kwa bar zote zinazoshiriki na wala sio baa chache zilizochaguliwa kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma”. Swai aliendelea kufafanua kwamba, washiriki watapimwa ujuzi wao katika kutayarisha nyama choma za aina tatu; nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi na nyama ya kuku.

 “Safari Lager tutaendelea kujitahidi kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora ya nyama choma. Tunawaomba sana washiriki kutumia vizuri elimu na uzoefu wanaopata ili kuongeza ubora wa utayarishaji wa nyama choma kwa wateja wetu. Mashindano haya ya Safari Lager Nyama Choma yatakosa maana sahihi endapo wachoma nyama watakuwa wanashiriki kwa lengo la kujipatia manufaa binafsi na kusahau yale yote waliyojifunza hadi mwaka mwingine”. Shindalo la mwaka huu linaongozwa na kibwagizo…. Safari Lager na Nyama Choma ndio Mpango mzima!. Alisema Swai.

Mwisho Swai  alitaja zawadi kwa kitongoji cha Dar One kuwa ni;
1.Bingwa wa Mkoa  ...............  Kikombe na nafasi ya kushiriki fainali ya Mkoa Leaders.
2.Mshindi  wa pili     ...............   Nafasi ya kushiriki fainali ya Mkoa Leaders
3.Mshindi wa tatu    ...............   Nafasi ya kushiriki fainali ya Mkoa  Leaders
4.Mshindi wa nne   ................   50,000/=
5.Mshindi wa tano  ................   50,000/=

0 comments:

Post a Comment