Thursday, March 12, 2015

 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Godwin Zacharia (katikati) akimkabidhi kikombe Mpishi Mkuu wa Bar ya SD Exective ya jijini Mwanza, Mussa Mashauri  mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya Safari Nyama Choma yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.Kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lger, Edith Bebwa.
.
Na Mwandishi Wetu.Mwanza.
SD EXECUTIVE Hotel jijini Mwanza wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2015 yaliyofanyiaka mswishoni mwa wiki katika Uwanja wa Furahisha na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja na Kikombe.
Nafai ya pili ilichukuliwa Gemestoni Bar ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 800,000/=,nafasi ya tatu ni Shooters Bar ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/=,nafasi ya nne ni Lunala ambayoilizawadiwa Shilingi 400,000/= na nafasi ya tano ni Victoria Prince Bar ambayo ilizawadiwa Shingi 200,000/-
Akizungumza na wakazi Mwanza walifika katika mashindano hayo, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Godwin Zacharia kwanza washukuru kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kwa kubuni mashindano hayo ambayo ni mwaka wa nane sasa mfululizo yenye mvuto wa pekee ambayo yanawapa picha halisi wakazi wa Mwanza kuwa wapi wanaweza kupata nyama choma bora kutoka katika baa tano ambazo zimeingia fainali katika jiji la Mwanza.
Alisema Zacharia kwanza kabisa tunawapongeza kwa kutoa elimu kwa wapishi wa baa mbali mbali za jijini Mwanza ambayo mliaanza nayo hapo awali tunaamini kwa kupitia  hilo wapishi wetu wameelimika si kama mlivyowakuta na hilo tunawashukuru na tunawaomba muendelee nalo kwani mnaongeza ajira kwa jamii kama si kupunguza umasikini.
Pili aliwapongeza baa tano zilizoingia fainali kwani wao ndio baa bora katika baa zote zinazochoma nyama mkoani humo na aliwaomba waendelee kuilinda hadhi na sifa hiyo waliyopewa katika jiji la Mwanza na mwisho aliwapongeza mabingwa wapya SD Exectuve Hoteli kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2015 na kuwaomba ambao hawakufanikiwa kupata nafasi hiyo wajiandae kwa mashndano yajayo ya Safari Nyama Choma 2016.
Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa aliwapongeza mabingwa wa mwaka 2015, SD Exective Hoteli na pia aliwashukuru wote walioshiriki toka mchakato ulipoanza mpaka kufikia kumpata bingwa lakini pia aliwashukuru wakazi wa Mwanza waliojitokeza kwa wingi kuja kushuhudia nani anatwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma 2015 jijini Mwanza.
Mwisho Edith aliwaomba washiriki wote ambao walipata zawadi wakatumie vyema zawadi walizopata kwa kuboresha majiko yao kwa mashindano yajayo ya 2016 lakini pia wakawe mabalozi wazuri wa bia ya Safari Lager kwenye biashara zao.

0 comments:

Post a Comment