Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Selestine Onditi(kushoto) akizindua rasmi
mashindano ya mchezo wa Darts Taifa yanayofanyika Moshi Hoteli Manzese jijini
Dar es Salaam leo.Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Darts Taifa(TADA),
Gesase Waigama.
Washiriki
wa mashindano ya Darts Taifa wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati
wa ufunguzi wa mashindano hayo yanayo fanyika Moshi Hotel Manzese jijini Dar es
Salaam
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Selestine Onditi(kushoto) akizindua rasmi
mashindano ya mchezo wa Darts Taifa yanayofanyika Moshi Hoteli Manzese jijini
Dar es Salaam.
Washiriki
wa mashindano ya Darts Taifa wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati
wa ufunguzi wa mashindano hayo yanayo fanyika Moshi Hotel Manzese jijini Dar es
Salaam
Washiriki
wa mashindano ya Darts Taifa wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati
wa ufunguzi wa mashindano hayo yanayo fanyika Moshi Hotel Manzese jijini Dar es
Salaam
Baadhi ya
washiriki wa mashindano ya Darts Taifa wakipasha kabla ya kuanza kwa mashindano
hayo yaliyofunguliwa Moshi Hoteli Manzese jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi
Wetu.
MASHINDANO
ya mchezo wa Darts Taifa yamezinduliwa jana jijini Dar es Salaam katika Hoteli
ya Moshi iliyopo Manzese kwa kushirikisha mikoa mitano ya Tanzania.
Akizindua
mashindano hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya kinondoni, Selestine Onditi ”kwanza
aliwapongeza viongozi wa chama hicho kwa juhudi za pekee za kufanya mashindano
hayo yafanyike kwa mwaka wa 2015,lakini zaidi aliwashukuru wachezaji kwa moyo
wa kupenda mchezo kujigarimia kuacha kazi zao kutoka mikoani ikiwa pamoja na
wenyeji Dar es Salaam kuja kushiriki mashindano hayo ya Taifa kwa kujilipia gharama zote za ushiriki hiyo
inatia moyo sana kuwa ni dhahiri mnaopenda mchezo”.
Alisema
Onditi michezo ni afya,michezo ni furaha na michezo ni kufahamiana basi
aliwataka washiriki wote watumie nafasi hii ya kukutana katika kuyafanikisha
haya yote.
Onditi
alitoa wito kwa wafadhili kuwa wasiegemee kwenye mpira wa miguu tu kuna michezo
mingi kama Darts na mingine wajitokeze wadhamini kwani kwa kutumia wapenda
michezo kama hawa waliojitolea kutoka mikoani kwa gharama zao kuja kushiriki
mashindano ya Taifa ni nafasi ya pekee
wewe mfanyabishara kutangaza biashara yako.
Mwisho
aliwatakia mashiondano mema yenye amani kuwa waanze salama na wamalize salama
na mwisho warejee majumbani salama salimini.
Nae
Mwenyekiti wa Chama cha Darts Taifa, Gesase Waigama alizitaja zawadi kuwa ni
Vikombe na Pesa taslimu kwa mfumo wa mashindano utakaotumika ni wa
Singles(mmoja mmoja), Doubles(wawili wawili) na Timu.
Mwisho
Katibu wa Chama cha Darts Taifa, Kalley Mgonja aliitaja mikoa iliyofanikiwa
kufika jijini Dar es Salaam kwa ushiriki wa mashindano ya Taifa kuwa ni Mbeya,
Morogoro, Dodoma, Arusha na wenyeji Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment