Friday, June 12, 2015

 Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI Tanzania Peter Zhang, akizungumza na waandishi wa habari juu ya uwekezaji katika Tekinolojia ya ICT nchini.Mazungumzo hayo yalifanyika Makao makuu ya HUAWEI Tanzania jijini Dar es Salaam.
 
 
Tarehe 18 na 19 Juni 2015, ndani ya ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) uliopo mkoani Dar es Salaam, kampuni ya Huawei Tanzania itashirikiana na Wizara ya mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kufanya kongamano la sekta ya Teknolojia ya IT. Kongamano hili litazungumzia teknolojia mpya ya IT ikiipa kipaumbele sekta mpya ya kuhifadhi data kwa kutumia njia ya mawingu.

Lengo na dhumuni ya kongamano hili ni kuendelea kuwawezesha Watanzania kwa njia moja au nyingine kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

kila mmoja wetu anaelewa  kua kwenye karne hii ya mawasiliano; teknolojia ya habari na mawasiliano ni muhimu sana hususani katika shughuli zetu za kila siku ziwe za kibinafsi au za kibiashara .

Kwa kupitia teknolojia ya Habati na Mawasiliano, dunia inakua zaidi na zaidi huku viwanda vilivyopo vikihitaji  kuhakikisha biashara inaendeshwa

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano imewezesha kwa kiasi kikubwa ukuaji wa sekta mbalimbali na kufanya ongezeko la uvumbuzi wa vitu mbalimbali na hivyo kupelekea kuongezeka kwa mahitaji ya ajira  hususani kwa upande wa vijana
Huawei Technologies Tanzania co. Ltd, imekua katika kiini cha mzunguko wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ulimwenguni ; ikiendesha shughuli zake katika kila nchi mbalimbali duniani. Huawei imejizatiti huku kuhakikisha kua kiongozi kwenye uvumbuzi wa teknolojia mpya pamoja na ukuaji na ongezeko la maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo, viwanda, biashara, ...... n.k

Kampuni ya Huawei Tanzania imewekeza nchini Tanzania kwa kiasi kikubwa na haswa  kwenye ukuaji wa maendeleo ya sekta ya Habari na Mawasiliano nchini. Katika sekta hii ya Habari na Mawasiliano, kampuni ya Huawei Tanzania imelenga Zaidi kwenye upande wa elimu na mawasiliano na imeahidi kuendelea kufanya hivo.

 

Mwaka 1998, Kampuni ya Huawei Tanzania ilianza shughuli zake nchini Tanzania na mpaka hadi leo ina wafanyakazi Zaidi ya 315 kupelekea kufanya idadi ya watanzania kua na Zaidi ya asilimia  75. Toka ianze shughuli zake za kukuza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini, Kampuni ya Huawei Tanzania imekua ikishikiriana na wadau wengine mbalimbali wa ICT ikiwemo  mashirika binafsi, mashirika ya uma pamoja na Serikali ya Tanzania.

Kampuni ya Huawei Tanzania inaongoza katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini Tanzania na imekua ikishirikiana na wadau wengine wa mawasiliano kama Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel na TTCL katika kuchangia ukuaji wa mmoja mmoja kwenye hii sekta (ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano).

0 comments:

Post a Comment