Friday, June 12, 2015

 
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Baraka Konisaga(wa pili kushoto) akimkabidhi mjasiliamali Jenereta wakati wa hafla ya kukabidhi Ruzuku kwa wajasiliamali 10 wa Kanda ziwa katika Programu Programu ya Safari Wezeshwa msimu wa nne inayoendeshwa na Bia ya Safari Lager.Kutoka kulia ni Mratibu wa program hiyo kutoka Kampuni ya TABDS, Veronica Mwamunyange, Maneja matukio wa Tbl Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela na Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa.

Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya Bia nchini kupitia Bia yake ya Safari Lager imekabidhi Ruzuku kwa Wajasiliamali 10 wa kanda ya Ziwa katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Furahisha mwishoni mwa wiki.
Wajasiliamali 10, waliokabidhiwa ruzuku hizo ni sehemu ya wajasiliamali 55 watakaowezeshwa nchini nzima katika Programu ya Safari Wezeshwa inayoendeshwa na Kampuni ya Tbl kupitia kinywaji chake cha Safari Lager.
Akizungumza na Wajasiliamali pamoja wageni waliojitokeza kwenye hafla ya makabidhiano ya Ruzuku hizo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga aliipongeza TBL, kupitia bia yake ya Safari Lager, kwa ubunifu mkubwa wa kuandaa program hii maalum ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo katika kuwainua kiuchumi inayojulikana kama “Safari Lager Wezeshwa”. Hivyo basi kuongeza fursa za ajira hapa nchini kupitia Ujasiriamali.  

Aidha Mkuu wa Wilaya aliwapongeza sana Wajasiriamali wote walioshiriki katika Programu  hii. Mvuto wa Wananchi wengi    kupenda    kuwa   Wajasiriamali   ni   jambo   jema, kwani litasaidia  sana  kukua  kwa  Sekta  Binafsi ambayo tunataka iwe Injini ya kuongeza ajira na Ukuaji wa Uchumi wetu.  Hivyo, nawapongeza sana na kuwatakia mafanikio Zaidi. 

Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa  aliwapongeza sana wajasiriamali waliofuzu katika programu ya “Safari Lager Wezeshwa” msimu huu wa nne. Jumla ya ruzuku za vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 220,000,000/= vitagawiwa kwa wajasiriamali 55 katika kanda nne za Tanzania. Kwa kanda hii ya Ziwa, tutashuhudia wajasiriamali 10 wa kanda hii wakikabidhiwa ruzuku zao na mgeni rasmi. 

Ruzuku hizi zinazotolewa katika program ya “Safari Lager Wezeshwa” msimu huu wa nne zinafanya jumla ya ruzuku zilizotolewa kufikia 620,000,000/=. Jumla ya wajasiriamali 157 wamefaidika moja kwa moja na programu hii, wananchi wengine wengi wanafaidika kutokana na wajasiriamali hawa kukuza biashara zao. Jumla ya ajira mpya kwa watanzania 361 zinategemewa kuongezeka hadi kufikia mwisho wa msimu huu wa nne. Hili ni ongezeko lao la ajira kwa asilimia 116%. 

Mwisho kabisa alitoa wito kwa wajasiriamali wote waliofaidika na mpango huu kuzingatia vizuri malengo ya program hiyo. Wafanye kazi kwa bidii na kujituma, maendeleo na kukua kwa biashara zao kuwanufaishe wao wenyewe, na jamii inaowazunguka. 

Kwa wajasiriamali ambao hawajafuzu msimu huu, wasikate tamaa, washiriki tena kwa kujaza fomu mapema na kwa usahihi msimu ujao. Wajasiriamali wanaofuzu wanapatikana bila upendeleo wowote na hawa wanaopokea ruzuku zao leo hapa ni mashahidi wetu katika hilo.

0 comments:

Post a Comment