Friday, June 12, 2015

Waremo wa kinywaji kipya cha Kill Twist wakishangilia boti ya kisasa iliyokuwa imebeba warembo wenzao na kinywaji hicho wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam. 
 
Waremo wa kinywaji kipya cha Kill Twist wakiwasili katika ufukwe wa Azura wakiwa na kinywaji hicho wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam.


 
Waremo wa kinywaji kipya cha Kill Twist wakishangilia mara baada ya wenzao kuwasili na boti ya kisasda ya kisasa iliyokuwa imebeba kinywaji hicho wakati wa uzinduzi uliofanyika katika Ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam.Kulia ni waandishi wa habari wakiwa kazini.

 
Waremo wa kinywaji kipya cha Kill Twist wakishangilia mara baada ya wenzao kuwasili na boti ya kisasa ya kisasa iliyokuwa imebeba kinywaji hicho wakati wa uzinduzi uliofanyika katika Ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam. 
Picha ya pamoja ya moja ya wageni waalikwa na warembo wa kill twist mara baada ya uzinduzi.

 
Baadhi ya stafu wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) wakiwa katika picha ya pamoja na  kinywaji cha kill twist mara baada ya uzinduzi uliofanyika katika ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam.KAMPUNI ya Bia nchini (TBL) leo hii imezindua bia mpya ya Kilimanjaro Twist (Kili Twist) yenye ladha ya machungwa. Hii ni mara ya kwanza kwa bia ya aina hii yenye ladha ya matunda kuzinduliwa hapa nchini.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Twist Edith Bebwa alisema, “Leo hii TBL imebadilisha mtazamo wa watu wanvyoifikiria bia kwa kuzindua kinywaji hiki. Hii ni bia ya kwanza ya ladha ya matunda humu nchini na tunatarajia kuwafikia wateja wengine ambao wanataka kuhisi kama wanakunywa bia lakini kupata ladha iliyolaini na tamu zaidi na ladha halisi ya machungwa”.

Bia ya Kilimanjaro Twist ni bia yenye asili ya Kitanzania kwa 100% na ladha halisi ya machungwa, ina kilievi cha asilimia 2 % tu . Bia hii inatengenezwa hapa nchini kwa kutumia viuongo vyenye ubora na ni mwanafamilia wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ni kati ya bia bora zaidi nchini.

Bia ya Kilimanjaro Twist itauzwa kwa bei ya TZS 1,500/= na itapatikana katika baa na hoteli zote kubwa za Dar es salaam. Kutokana na mtindo wa kimiminika cha bia hii, mnywaji anapta kiburudisho cha hali ya juu na hivyo inawaruhusu wanywaji kuinywa hata mida ya chakula cha mchana, wakati wa mapunziko nyumbani au ufukweni kitu ambacho bia za kawaida haziruhusu.

“TBL imekuwa mstari wa mbele katika maswala ya uvumbuzi ya viwanwaji vyake na tumeendelea kufanya hivyo na bia hii ya Kilimanjaro Twist inadhibitisha hilo. Nawasihi wateja waijaribu Kilimanjaro Twist kwani ina ladha nzuri na inastahili katika tukio lolote” alimalizia kwa kusema.

0 comments:

Post a Comment