Sunday, June 7, 2015

 Meneja wa Makao Makuu ya Kiwanda cha Bia Tanzania(TBL), Calvin Martin na Meneja wa Kinywaji cha Redd’s Original, Victoria Kimaro wakionyecha muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji hicho kwa wafanyakaji iliyofanyika Dar es Salaam
 Wafanyakazi wa Makao Makuu ya Kiwanda cha Bia Tanzania(TBL) wakiburudika na kinywaji cha Redd’s Original wakati wa hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original iliyofanyika Dar es Salaam
 Wafanyakazi wa Makao Makuu ya Kiwanda cha Bia Tanzania(TBL) wakiburudika na kinywaji cha Redd’s Original wakati wa hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original iliyofanyika Dar es Salaam

 Na Mwandishi Wetu.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo imezindua muonekano mpya wa kinywaji hicho ambacho kinapendwa na wanywaji wengi kutokana na ubora wake na ladha yake nzuri ya apple.  

Akizungumza na Wafanyakazi wa TBL, Dar es Salaam  wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa kinywaji cha Redd’s Original, Victoria Kimaro alisema leo tunazindua muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original kikiwa kwenye chupa bila kubadilisha chochote ndani yake ambapo itabaki na ubora  ulele,ladha ileile ila muonekano mpya ambao utawavutia wapenzi wa kinywaji hicho Zaidi. 

Alisema Victoria, muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original wa kwenye chupa utakuwa kwenye ujazo wa mililita 375 na kopo mililita 330 ambao utavutia wateja wengi wa kinywaji hicho.  

Kimaro alisema “Nia kubwa ni kuhakikisha tunampa mteja thamani yake halisi pale atakapokuwa anatumia kinywaji cha Redd’s Original na tunaendelea kuwahakikishia ubora wake utabaki kuwa wa kiwango cha juu kama ilivyo kawaida yetu,”. 

Meneja,Victoria aliomba wanywaji wa  Redd’s Original waendelee kukitumia kinywaji hicho kwani ni kinywaji bora zaidi kwa sasa kinachompa mteja nafasi kubwa ya kumthamini na kuutambua mchango wake.

0 comments:

Post a Comment