Friday, June 12, 2015

 
Baadhi ya washindi wa prpmosheni za Kilimanjaro waliowasili jijini Dar es Salaam kushuhudia  Kilimanjaro Tanzania Music Awards zinazotarajiwa kufanyka kesho katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Msham Isihakamwaka kutoka Mtwara, David Justin kutoka Mtawara na Robson Steven kutoka mkoani Mbeya.Tayari wako jijini Dar es Salaam kushuhudia Tuzo za Kilimanjaro kesho.
 Msham(kushoto) na David wakiwa katika Hotel ya Kebby's ambapo washindi wote wameandaliwa kufikia kwa maandalizi ya kushuhudia Tuzo za Kill.

Na Mwandishi Wetu.
WASHINDI waliopatikana katika Promosheni za Bia ya Kilimanjaro zilizofanyika nchini kote wameanza kuwasili jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo kushuhudia Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards. Hafla ya kukabidhi tuzo hizi inategemewa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi 13 June 2015.

Akizungumza na mwandishi wetu, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Bi. Pamela Kikuli amesema jumla ya washindi 22 wanatarajiwa kuwasili leo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania. Washindi hawa wataungana na washindi wengine 4 wa Hapa Dar Es Salaam. 

Bi. Pamela amesema washindi hawa walichaguliwa kwa njia ya kuponi baada ya wao kama wanywaji kununua bia ya Kilimanjaro kwenye Bar zilizokuwa na Promosheni. Washindi hawa wanalipiwa gharama zote za usafiri, Malazi na chakula kwa kipindi cha siku zote tatu watakazokuwa hapa jijini. 

Bi. Pamela amesema washindi wanaokuja ni kutoka katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Dodoma, Tanga, Mtwara, Mbeya, Kilimanjaro, Aruusha, Mwanza, Kahama, Musoma na Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment