Mratibu wa
Nanenane Kenice Pool Bonanza 2015 (88 Kenice Pool Bonanza 2015), Michael
Machellah(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati
wa kutangaza rasmi Bonanza hilo litakalofanyika jijini Dar es Saalaa.Katikati ni
Meneka wa Kampuni ya KENICE Tanzania, Eustace Masaki na Mwenyekiti wa waamuzi wa
mchezo wa Pool Taifa, Hashimu Shaweji.
Na Mwandishi
Wetu
KAMPUNI ya
kutengeneza meza za mchezo Pool ya KENICE imetangaza kudhamini Bonanza la
mchezo wa Pool utakaoshirikisha Mikoa saba katika kusherehekea Sikukuu ya
nanenane lijulikanalo kama “88 Kenice Pool Bonanza 2015.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Meneja wa Kampuni ya Kenice Tanzania Limited, Bwana
Eustace John Masaki alisema lengo la kufanya Bonanza hili ni kuendelea kuunga
mkono mchezo huu kwa pale ulipofikia ukizingatia
sisi ndio Mabingwa wa kutengeneza Meza zinazotumika katika mchezo huu hivyo
tumeona ni jambo jema na ni sehemu ya
pekee ya kukutanisha Vijana ambao ndio wachezaji wakuu wa mchezo huu
wakabadilishana mawazo kwa njia ya mchezo wa Pool kuliko kuwaacha wakizagaa
vijiweni.
Alisema
Masaki, tutambue mchezo wa Pool ni michezo kama michezo mingine na ukizingatia
michezo ni furaha,michezo ni afya na michezo ni ajira inayomfanya mtu yeyote
kupiga hatua katika maisha ukianzia na sisi kama Kampuni bila wachezaji wa pool
huko mitaani, hakuna wa kumuuzia hizi meza za pool tunazozalisha kila siku
ambapo itapelekea wafanyakazi tulionao kukosa ajira.Hivyo tunakila sababu za
kuunga mkono mchezo huu kuhakikisha unakua na unafaidisha jamii.
Masaki
alisema zaidi jumla ya Sh.Mil.6 tumetenga kwa ajili ya Bonanza hili
katika kusherehekea sikukuu ya nane nane kwa mwaka 2015.
Masaki
alizitaja zawadi za Bonanza hilo kuwa Bingwa atajinyakulia Meza ya Pool ya
kisasa kutoka Kenice yenye thamani ya Shilingi 2,000 000/= pamoja na pesa
taslimu Shilingi 300,000/=
Mshindi wa
pili atajinyakulia pesa taslimu Shilingi 500,000/=,mshindi wa tatu 300,000/= na
wa nne 100,000/=.
Patakuwa na
ushindani wamchezaji mmoja mmoja
(Singles) ambapo Bingwa atajinyakulia zawadi ya pesa taslimu Shilingi
200,000/=,mshindi wa pili 100,000/=,wa tatu 50,000/= na wane 30,000/=.
Nae mratibu
wa Bonanza hilo Bwana Michael Machellah alisema
Bonanza hilo litaanza Agosti 7,8 na kumalizika 9,2015 katika Ukumbi wa
CCM Mwinjuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam kwa kushilikisha vilabu vyote
vya mikoa ya kimichezo ya Ilala,Temeke,Kinondoni,Pwani, Morogoro, Iringa na
Dodoma.
Machellah alimaliza
kwa kutoa wito kwa vilabu vya mchezo wa Pool kujitokeza kwa wingi kuja
kushiriki Bonanza hilo la sikukuu ya nanenane.
0 comments:
Post a Comment