Wednesday, October 21, 2015

 Meneja Masoko TBL Fimbo Butallah na Meneja Mauzo wa Nzagamba Bw. Fred Kazindogo wakisoma jina la mshindi wa Zawadi ya Ng’ombe

Bia ya asili ya “Nzagamba” inayotengenezwa na kiwanda cha Nzagamba Mwanza, kilicho chini ya kampuni ya bia ya TBL imehitimisha promosheni yake ya “Jishindie Dume La Ng’ombe” kwa kukabidhi Zawadi hizo za Ng’ombe kwa washindi watatu katika mikoa ya Mwanza, Simiyu na Geita.
Zawadi hizo za Ng’ombe Dume ambao kwa lugha ya kisukuma hujulikana kama Nzagamba zimekuwa kivutio kikubwa kwa washindi na wananchi kwa ujumla kutokana na ukweli kuwa hii ni mara ya kwanza wananchi wameona kampuni ikifanya promosheni na kutoa Zawadi ya Ng’ombe, mara nyingi wamekuwa wakiona vitu tofauti lakini si ng’ombe. Tunawapongeza sana kampuni ya Nzagamba kwa ubunifu huu wa kutoa Zawadi za Ng’ombe, ni mawazo yanayofaa kuigwa, alisema mwananchi mmoja mkoani Mwanza.
Akiwataja washindi wa Zawadi hizo waliopatikana katika mikoa ya Mwanza, Simiyu na Geita Meneja wa Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Nzagamba Bw. Fred Kazindogo alisema; Tunayo Furaha kubwa kuweza kuwapata washindi wetu watatu wa zawadi hii kubwa ya Madume ya Ng’ombe. Mshindi wetu wa kwanza ni Ndugu Ibrahim Robert Shija, Mjasiriamali kutoka Kilimahewa,  Mwanza aliyepatikana siku ya Ijumaa tarehe 25 Septemba katika viwanja vya Kisesa, mshindi wa pili ni ndugu Kulwa Emanuel mkulima toka Bariadi, Simiyu aliyepatikana tarehe 26 Septemba na mshindi wa tatu ni Paschal Chrispine, dereva wa Dala Dala maeneo ya Nyankumbu, Geita aliyepatikana tarehe 27 Septemba. Washindi wote hawa tayari wameshakabidhiwa Zawadi zao za Ng’ombe Dume kila mmoja.

Nae meneja masoko wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bwana Fimbo Butallah alieleza jinsi promosheni hiyo ilivyoendeshwa hadi kufikia kupata washindi hao; Tulizindua promosheni hii tarehe 13 Agosti 2015 mjini Mwanza ikihusisha mikoa ya Mwanza, Simiyu na Geita, ambapo watumiaji wa bia hii ya Asili ya Nzagamba walitakiwa kununua bia, kisha kujaza kuponi iliyowawezesha kushiriki katika Bahati nasibu iliyotoa washindi hao. Tunafurahi sana kuona kuwa wananchi wamezipokea vizuri Zawadi hizi na hivyo tumehamasika zaidi kufanya promosheni kama hii kwa kila Mwaka. Tunawaahidi wananchi kuwa zawadi za Ng’ombe zitaongezeka ili kutoa fursa kwa washindi wengi zaidi kupatikana. Tunawaomba wananchi waendelee kuitumia Bia hii ya Asili ya Nzagamba inayotengenezwa kwa kutumia Mtama na Mahindi, mazao yanayolimwa hapa nyumbani.  Alisema Butallah 
 Zawadi ya Dume la Ng’ombe alilokabidhiwa mshindi wa Mwanza Bw. Ibrahim Robert Shija, katika viwanja vya Kisesa Sokoni.
 Mshindi wa Dume la Ng’ombe toka Mkoani Geita Bw. Paschal Chrispine akishukuru na kupongeza promosheni ya Bia ya Nzagamba katika hafla ya makabidhiano ya Zawadi iliyofanyika, soko la Nyankumbu, Geita
 Zawadi ya Dume la Ng’ombe aliyokabidhiwa mshindi wa Simiyu Bw. Kulwa Emanuel


0 comments:

Post a Comment