Saturday, October 17, 2015


Mkurugenzi wa Duka la Zizzou Fashion, Athumani Tippo (kushoto), akimkabidhi vifaa vya michezo kocha wa timu ya Changanyikeni Rangers, Steven Nyenge ndani ya duka hilo lililopo maeneo ya Sinza Afrikasana jijini Dar es Salaam.

DUKA la vifaa vya michezo la Zizzou Fashion mapema leo lilijitolea kutoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu ya soka ya Changanyikeni Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Pili.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkurugenzi Zizzou Fashion, Athumani Tippo alisema kwamba, amelazimika kutoa mchango wake kwa timu hiyo kutokana na kuonyesha juhudi, uwezo na kujituma kwa wachezaji wa timu hiyo kwa muda mfupi tangu ilipoanzishwa.
“Niameamua kutoa mchango wangu wa vifaa vya michezo kwa timu hiyo kwani imenishawishi baada ya kuifuatilia kwa muda sasa ambapo nimeziona juhudi za kocha wao, Steven Nyenge na wachezaji wote kwa ujumla wanavyojituma kuhakikisha wanapanda daraja,” alisema Tippo.
Tippo akiwa katika pozi na kocha wa timu ya Changanyikeni Rangers (katikati), na Kocha wa timu ya watoto ya Boko Beach Veterani, Maswanywa
 MOSHI VETERANI YAWACHAKAZA BOKO

Kikosi cha timu ya Boko Beach Veterani kikiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya mchezo huo kuanza.
 TIMU ya wakongwe ya Moshi Veterani Wikiendi iliyopita iliitembezea kichapo Boko Beach Veterani kwa bao 1-0 kwenye mechi ya kudumisha urafiki baina ya timu hizo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Boko jijini Dar es Salaam.
Nahodha  Moshi Veterani, Jafari Kiango (kushoto), akimkabidhi mchezaji wa timu ya Boko, Godfrey Malekano ‘Messi’,  zawadi ya Mchezaji Bora wa Mwezi kwa niaba ya Zizzou Fashion, muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

 
 

0 comments:

Post a Comment