Sunday, January 17, 2016

HARUNA NIYONZIMA 

Kiungo mchezaji huyu anaekipiga na Young Africans sports Club mabingwa wa ligi kuu mara 25 nchini Tanzania akitokea mjini Gisenyi nchini Rwanda, alizaliwa tarehe 5 February 1990.

Niyonzima ambaye kutokana na uwezo wake mkubwa kucheza kiungo cha juu na wing ya pembeni mashabiki wake wamembatiza jina na kumuita Fabregas wakimfananisha na kiungo wa Arsenal.

Kiungo huyu anaesifika kwa uwezo mkubwa wa kumiliki mipira, kutoa pasi nzuri za mwisho, kuitoa team kwenye mtego wa opponent inapopoteza uelekeo wa mashambulizi na kuirudisha safu ya ushambuliaji kwenye njia ya mashambulizi , ana urefu wa futi tano na nusu sawa na mita 1 na sentimita 67.

Mbali na kuichezea Yanga SC kama kiungo namba nane ama winger wa kushoto pia ni nahodha wa timu yake ya taifa ya Rwanda akisimama kama kiungo wa juu au attacking midfielder.

Safari ya soka ya mnyarwanda huyu inaanzia Etincelles nchini Rwanda aliyojiunga nayo mwaka 2005 akiwa kinda mdogo wa miaka 15 tu . Hapo ndipo alipoanza kuonesha uwezo mzuri wa kusakata soka akicheza kama namba 10 lakini kutokana na umbo dogo na nguvu hafifu ilimwia vigumu sana kuwika namba hiyo kutokana na kushindwa kupambana na mabeki . 
Mabosi wa Rayon Sports walimuona mchezaji huyu mwaka mmoja baadae na kumsajili katika kikosi chao chs vijana na kuanza kumtengeneza kama kiungo mchezeshaji na wakati mwingine kusimama kama mshambuliaji. Inside right au inside left.

Rwanda na viunga vyake vilianza kusikia sifa za kiungo huyu pale alipoanza kuibeba Rayon mabegani mwake kwa uwezo mkubwa eneo la kiungo cha juu.

APR wakiwa na jeuri ya pesa waliinasa sahihi ya kiungo huyo na kumpa kandarasi ya miaka 4 . Akiwika na APR ndipo hata makocha wa Amavubi walipomuona vyema na kuanza kumtumia mwaka 2007.

Licha kucheza soka la kulipwa nchini Tanzania ambapo ligi yake haijaendelea sana kama ligi zingine barani Afrika, Niyonzima anaheshimika sana nchini Rwanda pengine kuliko yoyote ndani ya kikosi cha Amavubi.

Anahesabika kama balozi wa soka la Rwanda nje na ndani ya Rwanda.

APR hawakuweza kudumu sana na kiungo huyo baada ya kucheza misimu mitatu tu , 2007/8, 2008/9, 2009/10 na walipokuja kwenye michuano ya Challenge mwaka 2011 ndipo Yanga walipomuona na kumnunua kiungo huyo. Timu ambayo ameichezea kwa mafanikio makubwa hadi sasa.

Akiwa na Yanga SC alifanikiwa kuibuka mchezaji bora msimu wa 2012/13.

Akiwa na Yanga ameweza kuvaa medali ya ubingwa VPL 2012/13 na 2014/15 akiwa pia na medali tatu ngao ya jamii.

Huyo ndio mkali wetu wa siku Haruna Niyonzima anaekipiga na Wanajangwani. 

Samuel Samuel

0 comments:

Post a Comment