Thursday, March 31, 2016

 Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo Bw. Robert Pascal wakifuatilia mada wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Robert Pascal (Kulia) akiwasilisha Mada kuhusu Wajibu wa TADB katika kuendeleza kilimo nchini wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam.

 Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo, na Uvuvi, Mhe. William Ole Nasha (Kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Wapili kulia) wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania, Bibi Janet Bitegeko ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB.

 Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo, na Uvuvi, Mhe. William Ole Nasha (Kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania, Dkt. Sinare Yusuf Sinare (Kushoto) na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Wapili Kushoto) wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam.

 Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania, Dkt. Sinare Yusuf Sinare (Wapili kushoto) akizungumza na Balozi wa Norway nchini, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad (Kushoto) wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo, na Uvuvi, Mhe. William Ole Nasha (Kulia), Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Wapili kulia) na Afisa Mtendaji  Mkuu-SAGCOT, Bw. Geoffrey Kirenga.

 Mbunge wa Babati Vijijini, Mhe. Jitu Soni (Kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Robert Pascal (Katikati) wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mmoja wa wadau waliohudhuria warsha hiyo.

 Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo, na Uvuvi, Mhe. William Ole Nasha (Kulia) akiagana na  Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Katikati) na Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania, Dkt. Sinare Yusuf Sinare (Kushoto) mara baada ya kufungua Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Wapili Kushoto) akizungumza na Mbunge wa Babati Vijijini, Mhe. Jitu Soni (Kulia) wakati alipotembelea Meza ya TADB wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania, Dkt. Sinare Yusuf Sinare (Wapili kulia) na Afisa Maendeleo ya Biashara Mwandamizi wa TADB, Bw. George Nyamrunda.

 Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Saidi Mkabakuli akitoa maelezo ya kuhusu TADB kwa mmoja wa wadau waliotembela Meza ya TADB wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam.  Mbunge wa Babati Vijijini, Mhe. Jitu Soni (Kulia) akioneshwa moja ya bidhaa zilizokuwa zikioneshwa katika Meza ya TADB wakati wa Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Anayemuonyesha ni Afisa Maendeleo ya Biashara Mwandamizi wa TADB, Bw. George Nyamrunda.


Na Mwandishi wetu,
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria kusaidia upatikanaji wa Masoko ili kuongeza Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini ili kuchagiza na kusaidia kuwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini.

Akizungumzia katika Warsha ya Kitaifa ya Wadau ya Sekta ya Kilimo inayofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam, yenye Mada Kuu ya Warsha hiyo,Wazalishaji Tuanze na Soko, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi amesema kuwa ukosefu wa masoko ya mazao unaowakabili wakulima umekuwa ni moja ya changamoto kuu zinazorudisha nyuma maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.

Bw. Samkyi amesema kuwa ili kusaidia kutokomeza changamoto hiyo na nyinginezo Serikali iliamua kuanzisha TADB ili kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa mikopo na masoko katika sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika kilimo nchini.
“Katika kutekeleza majukumu yetu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania imeanza huduma zake kwa kulenga minyororo michache ya ongezeko la thamani katika kilimo ambapo  mikopo ya aina mbalimbali hutolewa kuwezesha wakulima kuongeza tija na uzalishaji katika sekta ya kilimo nchini Tanzania,” alisema Bw. Samkyi.

Kwa mujibu wa Bw. Samkyi, Benki inatoa mikopo kwa ajili ya uwekezaji kwenye  ujenzi viwanda vya kusindika mazao, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya usindikaji wa mahindi na kuongeza thamani, ununuzi wa vifaa vya uvunaji wa kisasa wa mahindi, vifungashio vya kisasa vya kuhifadhia mahindi na teknolojia ya uhifadhi wa mahindi kupunguza upotevu wa mazao.
“Kwa sasa tumejikita katika mnyororo mzima wa uongezaji wa thamani kuanzia uandaaji wa shamban hadi kwa upatikanaji wa masoko, ikiwemo mahitaji ya uzalishaji wenye tija kwenye sekta nzima ya kilimo kuanzia hatua za awali za utayarishaji wa mashamba, kupima ubora wa udongo na virutubisho vinavyohitajika kwenye uzalishaji wa mahindi, upatikanaji wa pembejeo za kilimo zikiwemo mbegu bora, mbolea, madawa na vifaa na teknolojia mbali mbali za umwagiliaji na fedha kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali za uzalishaji wa mahindi,” aliongeza.

Mkurugenzi Samkyi, ameongeza kuwa Benki imejipanga kutoa mikopo ya ununuzo wa mitambo na mashine za ukaushaji, usafishaji na uchambuzi wa madaraja ya mahindi pamoja na mitambo ya usindikaji na usagaji wa nafaka na ujenzi wa viwanda vya kusindikia mazao ikiwamo fedha kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali za uendeshaji katika kuongeza thamani ya mazao
Pia, Benki inatoa mikopo kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya kilimo katika kuimarisha minyororo ya thamani katika kilimo ambapo inajumuisha ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na mitambo ya umwagiliaji, uchimbaji wa visima vya maji ya umwagiliaji, ujenzi wa mabawa ya uvunaji maji ya mvua, ujenzi wa maghala bora ya kuhifadhia mahindi na ujenzi wa miundombinu ya masoko.

Akizungumzia aina ya mikopo itolewayo na benki hiyo, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo Bw. Robert Pascal amesema kuwa Benki inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya muda mfupi (Short term loans), mikopo hii ni ya muda mfupi usiozidi miaka miwili (au miezi 24), Mikopo ya muda wa kati (Medium term loan), mikopo ya muda wa kati hutolewa kwa kipindi cha miaka 2 hadi 5 (yaani kati ya miezi 24 na 60) na Mikopo ya muda mrefu, mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kugharamia shughuli za uwekezaji mkubwa kwenye kilimo na ambazo marejesho yake yatafanyika katika kipindi cha miezi 60 hadi 180 (yaani kati ya miaka 5 hadi 15).

Bw. Pascal ameongeza kuwa riba itozwayo kwa upande wa Mikopo ya muda mfupi (Short term loans) ni riba ya asilimia saba (7%) mpaka (8%) kwa mwaka. Ambapo mikopo hii Hutolewa kwa ajili ya kufanikisha shughuli za kilimo kwenye mnyororo wa thamani. Kwa mfano, kugharamia shughuli za kilimo zinazofanywa kabla ya mazao kuvunwa, na mara baada ya kuvunwa, ununuzi wa mazao, ununuzi wa zana na mashine za kilimo na mahitaji mengine ya kifedha katika mnyororo wa thamani.

Ameongeza kuwa mikopo ya muda wa kati hutolewa kwa kipindi cha miaka 2 hadi 5 (yaani kati ya miezi 24 na 60) na hutozwa riba ya asilimia tisa (9%) mpaka (10%) kwa mwaka. Na mikopo hii hutolewa ili kufanikisha mahitaji maalumu, mathalani: kupanua mashamba,          kuzalisha aina mpya za mbegu, mifugo, na samaki na kuongeza kiwango cha rasilimali au uwekezaji, kuboresha miundombinu, pamoja na kuziba pengo la mahitaji mengine ya muda wa kati kwenye mnyororo wa thamani. 

Na kwa upande wa Mikopo ya muda mrefu hutozwa riba ya asilimia kumi na moja (11%) mpaka (12%). Mikopo hii hutolewa kugharamia mahitaji ya muda mrefu, mathalani: gharama za kupata rasilimali, kujenga miundombinu mikubwa ya kilimo, kupanua mashamba makubwa na ya kati, pamoja na shughuli nyingine za  kilimo zinazohitaji mikopo ya muda mrefu. Mikopo ya muda mrefu inalenga kufanikisha uwekezaji kwenye miradi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na mahitaji mengine ya muda mrefu.
“Mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kujenga/kukarabati miundombinu katika sekta ya kilimo kwenye mnyororo wa thamani, kwa mfano: skimu/mifumo ya umwagiliaji, maghala ya kisasa ya kuhifadhia mazao, pamoja na mahitaji mengine ya miundombinu ya kilimo,” aliongeza Bw. Pascal. 

TADB ilianzishwa kwa Sheria Namba 5 ya mwaka 2006 inayosimamia Benki na Taasisi za Fedha, pamoja na Kanuni za Uanzishaji wa Benki na Taasisi za Fedha (Development Finance) za mwaka 2012. Lengo la msingi la kuanzishwa kwa TADB ni kutoa mikopo ya muda mfupi, kati na muda mrefu kwa sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi ya kilimo nchini.

0 comments:

Post a Comment