Monday, March 21, 2016

 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dr.Frida Mokiti(wa pili kulia) akikata utepe wakati wa ufunguzi wa Tawi jipya la Bima ya Afya ya Kampuni ya Resolution Insurance jijini Arusha mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja wa Kampuni hiyo chini, Oscar Osir na Meneja wa Tawi wa la Arusha, Lucas Msomi.

Na Mwandishi Wetu,Arusha
MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dr.Frida Mokiti amewashauri wakazi wa jiji la Arusha kujiunga na Bima ya Afya ya Resolution Insurance katika uzinduzi wa Tawi jipya lililofanyika mwishoni mwa wiki  katika jingo la NSSF – Mafao House nan baadae chakula cha jioni katika Hoteli ya Maunt meru.
Dr.Frida kwanza aliipongeza Kampuni ya Resolution Insurance kwa kufungua tawi jipya jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya kuwasogezea huduma wakazi wa Arusha pamoja na wateja wao waishio Arusha.
Alisema Dr.Frida, Bima ni muhimu sana kwa kila binadamu hasa katika maisha ya sasa yenye mlipuko wa magonjwa mengi, nifulsa yenu sasa wakazi wa Arusha kutumia nafasi hii.
Nae Manager wa Resolution Insurance Tanzania, Oscar Osir alisema wamejipanga vizuri katika kutoa huduma hii ya Bima ya Afya kwa watanzania nchini kote na sasa wako katika hatua ya kusogeza huduma hii kila mkoa ndio maana sasa wamesogea Arusha.
Oscar alisema ni nafasi ya pekee sasa wakazi wa Arusha kutumia fursa hii ya Bima ya Afya kutoka Resolution itakayohakikisha kukupa huduma stahiki na nzuri zaidi.
Resolution Insurance ni Kampuni pekee ya Bima ya Afya  inayoongoza East Afrika.


Mganga Mkuu wa Mkoa wa  Arusha, Dr.Frida Mokiti(kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya Afya ya  Resolution Insurancena pamoja na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi tawi jipya la Kampuni hiyo katika jingo la NSSF Mafao House mwishoni mwa wiki mkoani Arusha.
 Meneja wa Kampuni ya Bima ya Afya ya Resolution Insurance, Oscar Osir(kulia) akizungumza na wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa ufunguzi wa tawi jipya la Kampuni hiyo jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

 Kocktail0 comments:

Post a Comment