Tuesday, March 1, 2016



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Kushoto) akiangalia ramani ya Zahanati na Nyumba ya wafanyakazi mara baada ya  mkutugenzi mtendaji
wa kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Bruce Zhang (Kulia) kutoa msaada wa kompyuta 25 na UPS 25 kwa shule tano za
sekondari pamoja na kuzindua ujenzi wa mradi wa Zahanati ya kijiji cha
Nandagala wilayani ya Ruangwa utakaojengwa na Kampuni hiyo.



Na Mwandishi Wetu- Ruangwa Lindi.

KAMPUNI ya Huawei Technologies (Tanzania) Co. LTD leo imetoa msaada wa
kompyuta 25 na UPS 25 kwa shule tano za sekondari pamoja na kuzindua
ujenzi wa mradi wa Zahanati ya kijiji cha Nandagala wilayani ya
Ruangwa.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa alikuwa mgeni rasmi wa tukio hilo ambalo
pia limehudhuliwa na mkutugenzi mtendaji wa kampuni ya Huawei Tanzania
Bw. Bruce Zhang.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo katika kijiji cha
Nandagala, wilaya ya Ruangwa jana, Waziri mkuu Kassim Majaliwa
alipongeza uamuzi wa kampuni hiyo kusaidia jamii ambayo ilikuwa
ikikabiliwa na changamoto mbali mbali.

Alisema kuwa wakazi wa wilaya ya Ruangwa walikuwa na changamoto mbali
mbali za ikiwemo utoaji wa mafunzo ya vitendo ya teknolojia ya habari
na mawasiliano (Tehama) kwa wanafunzi wa sekondari na pia kukosekana
kwa huduma muhimu za kijamii ikiwemo afya.

Waziri Mkuu alishukuru kampuni hiyo na kusema kuwa kompyuta hizo ni
muhimu kusaidia shule za sekondari  kufundisha wanafunzi kwa vitendo
ili waweze kuendana na ukuaji wa teknolojia.

Alisema kuwa Tanzania itaendelea kujenga mahusiano na serikali ya
China pamoja na makampuni kutoka nchini humo hasa katika sekta ya
teknolojia ya habari na  mawasiliano kwa kuwa sasa serikali imeingia
mkataba na kampuni ya Huaweei kama mshauri mkuu wa masuala ya Tehama.

“Tunashauri makampuni mengine ambayo yamewekeza Tanzania kuwa na
mikakati ya kusaidia jamii, kwa kuonyesha nia yao njema kwa wananchi
wanao wahudumia ili kuwezesha biashara zao kukua na kuleta imani kwa
wananchi,” alisema.

Mkurugenzi mtendaji wa Huawei Technologies Tanzania, Bruce Zhang
alisema kampuni yake imewekeza atika teknolojia kwa kuwawezesha vijana
wa wakitanzania kupata uzoefu, na kuleta mabadiliko chanya ya katika
teknolojia ya habari na mawasiliano.

Alimwambia waziri mkuu kuwa Huawei wanajitolea katika kuchangia
shughuli mbali mbali za maendeleo na kwa zaidi ya miaka 15 sasa
kampuni hiyo imetoa misaada mbali mbali ikiwemo ujenzi wa hospitali,
shule na misaada mingine.

“Kwa zaidi ya miaka 15 sasa, Huawei imekuwa pamoja na watanzania kwa
kuwaezesha wazawa kupata ujuzi na teknolojia, hivyo nchi kama Tanzania
inahutaji kuwa na wawekezaji kama Huawei wanao wanufaisha watanzania,”
alisema.

Alisema mbali na kutoa vifaa vya teknolojia ya habari na mawasiliano
Huawei imekuwa mdau mkubwa katika ujenzi wa mkongo wa taifa na
kusaidia katika miladi ya elimu kwa njia ya kielektroniki.

“Kampuni yetu imeweze kutoa mafunzo ya Tehama kwa waajiri wake ambapo
hadi sasa wengi ni watalaam katika tasnia hii, tumewezesha taasisi
nyingi za elimu ya juu kutumia teknolojia pia misaada mbali mbali
imetolewa katika mashule, Zahanati na kwa watanzania kwa ujumla,”
alisema..

Alisema kuwa kampuni yake inaamini kuwa shirika lolote binafsi
linaweza kukua endapo litashirikiana moja kwa moja na wananchi kwa
kuwaongezea ujuzi kutokana na shughuli wanazofanya.

Aliongeza kuwa mpaka sasa kampuni hiyo imeajiri zaidi ya wafanya kazi
230 ambapo kati yao 155 ni watanzania na 75 ni raia kutoka China na
nchi za jirani, hivyo idadi ya watanzania walioajiliwa katika kampuni
hiyo ni sawa na asilimia 67 ya waajiriwa wote.

0 comments:

Post a Comment