Saturday, April 9, 2016Balozi wa Samsung, Elizabeth Kimaro (katikati) akizungumza na wateja wakati wa Promosheni ya toleo jipya la simu ya Samsung Galaxy S7 Mlimani City Dar es Salam.Simu hiyo inapatikana katika maduka ya Samsung Nchini kwa sasa.

 Balozi wa Samsung, Jesca Abbas (kulia) akizungumza na wateja wakati wa Promosheni ya toleo jipya la simu ya Samsung Galaxy S7 Mlimani City Dar es Salam.Simu hiyo inapatikana katika maduka ya Samsung Nchini kwa sasa.

 Moja ya wateja wa Samsung Galaxy S7 akiangalia muvi(video) kwa kutumia kifaa maalum, Gear VR wakati wa Promosheni ya toleo jipya la simu ya Samsung Galaxy S7 Mlimani City Dar es Salam.Simu hiyo inapatikana katika maduka ya Samsung Nchini kwa sasa.

 Na Mwansishi Wetu.
KAMPUNI  ya Samsung Nchini imeingiza sokoni simu mpya ya Samsung Galaxy S7 yenye vivutio lukuki vya kukufanya Dunia uione iko kiganjani.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja mafunzo wa bidhaa za Samsung, Julius Giabe mara baada ya uzinduzi alisema simu ya Samsung Galaxy S7 ni toleo jipya ambalo kwa sasa inapatikana madukani kote nchini.
Amewaomba watanzania wajitokeze kununu simu hiyo yenye ubora wa hali ya juu kwani imeboreshwa zaidi kulingana na tekinolojia ya sasa.
Alisema  Julius Samsung Galaxy S7 imeboreshwa zaidi kwenye upande wa Camera kwani ina Mega Pixel 12 zilizoboreshwa zaidi kiasi ambacho unaweza kupata picha au Video nzuri zaidi.
Kioo chake kizuri cha kuvutia na inazuia vumbi na Maji kwa muda wa dakika 30 ndani y maji.
Julius alisema, Samsung Galaxy S7 inakaa na chaji kwa muda mrefu sana na hata ikiisha chaji inauwezo wa kuichaji bila kuchomeka kwenye Umeme(Wireless charging)
Julius alimaliza kwa kuwaomba watanzania tusikose kumiliki simu ya Samsung Galaxy S7 ukakosa mambo mazuri katika teknolojia hii ya kisasa ambayo Dunia yote iko Kiganjani mwako.
Kwa wakazi wa Dar es Salaam tutembelee Mlimani City ambapo promosheni ya Samsung Galaxy S7 inaendelea,upate kwa undani ubora wa simu hiyo.
“Kuwa wa kwanza kumiliki simu ya Samsung Galaxy S7”. Wateja mbalimbali wakipata maelekezo ya kina toka kwa mabalozi wa Samsung Galaxy S7 wakati wa Promosheni ya simu hiyo inayoendelea Mlimani City jijini Dar es Salaam. Simu hiyo inapatikana katika maduka ya Samsung Nchini kwa sasa.
Mabalozi wa Samsung Galaxy S7 wakipata picha (Selfie) kwa kutumia simu ya Samsung Galaxy S7 wakata Promosheni ya simu hiyo inayoendelea Mlimani City jijini Dar es Salaam. Simu hiyo inapatikana katika maduka ya Samsung Nchini kwa sasa.

0 comments:

Post a Comment