Wednesday, August 10, 2016


Baadhi ya Mashabiki na wachezaji wa Pool wa Klabu ya Topland yenye makazi yake Magomeni Kinondoni  wakiwa wamembeba Nahodha wa klabu akiwa na kikombe mara baada ya kibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Pool ya siku kuu ya Nane nane yaliyojulikana kwa “88” Pool Competitions 2016, yaliyo malizika juzi wakati wa siku kuu hiyo katika Viwanja vya Bashnet Mtongani jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya Mashabiki na wachezaji wa Pool wa Klabu ya Topland yenye makazi yake Magomeni Kinondoni  wakishangila na kikombe mara baada ya kibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Pool ya siku kuu ya Nane nane yaliyojulikana kwa “88” Pool Competitions 2016, yaliyo malizika juzi wakati wa siku kuu hiyo katika Viwanja vya Bashnet Mtongani jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Isaach Togocho(kulia) akimkabidhi kikimbe nahodha wa klabu ya Topland ya Magomeni Kinondoni, Patrick Nyangusi mara baada ya ya kibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Pool ya siku kuu ya Nane nane yaliyojulikana kwa “88” Pool Competitions 2016, yaliyo malizika juzi wakati wa siku kuu hiyo katika Viwanja vya Bashnet Mtongani jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Isaach Togocho(kulia) akimkabidhi pesa taslimu Shilingi laki tano nahodha wa klabu ya Topland ya Magomeni Kinondoni, Patrick Nyangusi mara baada  ya kibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Pool ya siku kuu ya Nane nane yaliyojulikana kwa “88” Pool Competitions 2016, yaliyo malizika juzi wakati wa siku kuu hiyo katika Viwanja vya Bashnet Mtongani jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni, Mathayo Makemba.

Bingwa wa Singles, Issa Selemani akikabidhiwa zawadi yake.

Na Mwandishi Wetu.
TIMU ya Topland yenye makazi yake Magomeni, Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam wameibuka mabingwa katika mashindano ya mchezo wa Pool yajulikanayo kama “88” Pool Competitions 2016  baada ya kuwafunga timu ya Dodoma 13 – 4, na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi  laki tano (500,000/=) na Kikombe.

Topland walitwaa ubingwa huo katika mashindano hayo yaliyoshirikisha Vilabu 16 vya mchezo wa Pool kutoka mikoa mbali mbali.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Dodoma ambao walizawadiwa pesa taslimu Shilingi laki mbili na nusu(250,000).Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Klabu ya Fuoni kutoka Zanzibar ambao  walishinda kwa kuwafunga klabu ya Sunset 13 – 5 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu shilingi laki moja na nusu(150,000) na nasafi ya nne ilichukuliwa na Sunset ambao walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi elfu hamsini(50,000).

Upande wa mchezaji mmoja mmoja (Singles), mchezaji Issa Selemani kutoka Klabu ya Mpo Afrika Ilala aliibuka kuwa bingwa baada ya kumfunga Hussein Madroback kutoka Klabu ya Kayumba ya Mkoa wa kimichezo ya Ilala 5 – 3, na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi laki mbili (200,000) pamoja na ngao.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Hussein Madroback ambaye alizawadidiwa pesa taslimu shilingi laki moja(100,000).Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Merczedec Amadeus bada ya kumfunga Abdul Faraji kutoka Dodoma 4 – 2, na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi elfu hamsini na Abdu Faraji kujitwalia nafasi ya nne ambapo alizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi elfu ishirini na tano (25,000).

Klabu shiriki katika mashindano hayo zilikuwa ni pamoja na Klabu ya Fuoni kutoka Zanzibar, Mpo Afrika kutoka Temeke, Kayumba kutoka Ilala, Sunset kutoka Temeke, Topland kutoka Kinondoni, BMK kutoka Temeke, Y2K kutoka Ilala, Mboya kutoka Kilimanjaro, Jaba kutoka Kinondoni, Soccer City kutoka Kinondoni, Tabata kutoka Ilala, Kurasini City kutoka Temeke, Mbezi Beach Inn kutoka Kinondoni, MKWAJUNI KUTOKA Kinondonmi na Dodoma  kutoka Dodoma.

Akizungumza na wachezaji pamoja na mashabiki wakati wa kukabidhi zawadi, Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa Chama cha Pool Tanzania, Isaach Togocho aliwapongeza waandaaji wa mashindano ya Pool nanenane ambayo yalijulikana kama “88” Pool Competitions 2016 kwa kufanikisha mashindano hayo kwa ubora wa juu na hamasa kubwa na kuwaomba wadau wengine kuiga mfano huo ambao utafanya mchezo kusonga mbele.

Aidha Togocho aliwaomba wachezaji na washika dau kuhakikisha wanakemea wale wote wanaosababisha kuonekana mchezo wa pool kuonekana wa kihuni hususana wacheza Kamari ambao hawafuati hata sharia ya nchi ya muda maalumu wa kucheza mchezo huo hata ikibidi kuwapeleka kwenye vyombo vya sharia.

0 comments:

Post a Comment