Monday, August 22, 2016

 Muimbaji wa Bendi ta TOT, Abdul Misambano akiimba sambamba na waimbaji wengine wakati wa onyesho lao la kila ijumaa katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Rapa wa Bendi ya TOT, Issa Sadi akiimba sambamba na wanenguaji wa bendi hiyo wakati wa onyesho lao la kila ijumaa katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Na Mwandishi Wetu.
BENDI ya TOT yenye makazi yake Mkuu CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam, imekuja kivingine mara baada ya pilika pilika za Chama cha Mapinduzi kumalizika kwa kutoa burudani kwa wapenzi na mashabiki wa Dansi na Taarabu katika Ukumbi wao wa CCM Mwinjuma kila Ijumaa ikiwa ni sehemu ya kuihakikishia jamii kuwa hawako kichama tu bali kuna maisha baada ya Chama.

Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa Bend Frank Kabatano alisema kwa sasa TOT Bandi na Taarabu tuko katika maisha mengine kabisa baada ya siasa kumalizika.Tumeanza na ukumbi wa nyumbani kwa sasa kila ijumaa tutatoa burudani mbili kwa pamoja yaani Taarabu na Mziki wa Dansi yote hiyo ni katika kuwahakikishia wapenzi kuwa hatuko kwa ajili ya Chama tu bali hata jamii nzima bila kujali kabila jinsia wa itikadi.

Alisema Kabatano, TOT Band kwa sasa inatamba na nyimbo zake mpya kama; Wivu utunzi wake Abdul Misambano, Pilipili utunzi wake Msemaji wa Bendi Frank Kabatano, Acha kulia utunzi wake J4,  Afidhi utunzi wake Athanas Monthanabe na zingine nyingi.
Wakati upande wa Taarabu ukiongozwa na Malkia wa Mipasho Tanzanaia, Khadija Koppa akitamba na nyimbo zake mpya kibao bila kuacha nyimbo yake ya “Naheshimu kazi yangu ndio inayoniweka mjini” utunzi wake mwenyewe na zingine nyingi.

Alisema Kabatano, ni wakati sasa wa wapenzi wa Taarabu na mziki wa Dansi kuja kuona na kusikiliza burudani kutoka TOT ili upate radha nyingine ya pekee ambayo hujawahi kupata.

Wiki hii Bandi ya TOT wakatakuwa kiwanja cha nyumbani tena CCM Mwinjuma, Mwananyamala na wakati huo huo jumapili watakuwa na Bonanza hapo hapo CCM Mwinjuma.
 Waimbaji wa Taarabu wa Bendi ya TOT wakicheza wakati wa onyesho lao la kila ijumaa katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wanenguaji wa Bendi ya TOT wakicheza wakati wa onyesho lao la kila ijumaa katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

0 comments:

Post a Comment