Thursday, September 15, 2016

 Asifa mnadhimu wa Jeshi la Polisi Nchini, Kamishna Mwandamizi wa Polisi Fortunatus  Musilimu akiwakabidhi Oil za Total 4T madereva boda boda mala baada ya uzinduzi rasmi wa vilainishi hivyo.Hafla ya Uzinduzi ilifanyika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam.
 Asifa mnadhimu wa Jeshi la Polisi Nchini, Kamishna Mwandamizi wa Polisi Fortunatus  Musilimu akiwakabidhi Kofia maalumu za kuendeshea Pikipiki(Helmeti) madereva boda boda mala baada ya uzinduzi rasmi wa vilainishi vya Tatal 4T.Hafla ya Uzinduzi ilifanyika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam.
Asifa mnadhimu wa Jeshi la Polisi Nchini, Kamishna Mwandamizi wa Polisi Fortunatus  Musilimu akiwa kwenye picha ya pamoja na madereva Bodaboda mara baada ya uzinduzi wa vilainishi maalumu vya Pikipiki na bajaji vya Tatal 4T.Hafla ya Uzinduzi ilifanyika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam.

Total Tanzania yazindua  bidhaa mpya “Special 4T”, kilainishi mahsusi kwa ajili ya pikipiki na bajaji.
Katika harakati za kuwafikia wateja wake wote, kwa kuwapa huduma na bidhaa zenye uhakika, Total Tanzania imezindua kilainishi  kipya nchini, kijulikanacho kama Special 4T,  ambacho ni mahususi kwa ajili ya pikipiki na bajaji zenye “4 stroke engine”.

Kilainishi hiki cha SPECIAL 4T  hulinda injini ya bodaboda na bajaji, na kuzuia  msuguano kati ya vipuri na kifanya injini kuwa nyepesi na mwendo wa kasi pia kuiwezesha kufanya kazi kwa muda mrefu Zaidi bila kuharibika. Hivyo kuwasaidia wamiliki wa bajaji na bodaboda kupunguza gharama ya kufanya matengenezo  mara kwa mara. Tunawashauri wamiliki wa Bodaboda na Bajaji watumie kilainishi hiki cha SPECIAL 4T ya TOTAL ambacho kitawawezesha kufanya safari za umbali wa kilomita kati ya 2200 mpaka 2500 bila kubadilisha ( Oil drainage period)
Uzinduzi huu wa bidhaa mpya ni matokeo ya utafiti uliofanywa na wataalamu wa kampuni ya TOTAL kwa baadhi ya waendesha bodaboda na bajaji na kugundua kuwa madereva na wamiliki wengi hutumia vyombo vyao kwa biashara hivyo hutembea umbali mrefu na kufanya injini kuchakaa na kuwa dhaifu mara kwa mara kwa kutumia vilainishi visivyo na viwango bora. Hivyo hutumia gharama kubwa zaidi kufanya matengenezo

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Meneja  Mauzo wa Vilainishi na bidhaa maalumu za Total, Bwana Anam Mwemutsi alisema; “lengo letu ni kumsaidia mmiliki wa  bodaboda na bajaji kuweza kufanya biashara zake kwa gharama nafuu bila hofu ya kuharibika kwa injini. Tumeleta kilainishi ambacho hakitamlazimu kufanya matengenezo  kwa chombo chake mara kwa mara, kwa sababu itamruhusu kutembea kilometa nyingi bila kubadilisha.  Na kutokana na  ubora wa bidhaa zetu, tunamhakikishia mteja uimara na ulinzi kamili wa injini yake wakati wowote na kwenye barabara yoyote ile Tanzania nzima“

Bidhaa hii ya SPECIAL 4T itapatikana katika vituo vyote vya mafuta vyaTotal na kwa mawakala wetu waliothibitishwa nchi nzima.
“Ningependa kuwashukuru Total kwa kuja na bidhaa hii. Kwa ubora wake utasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara kwa waendesha pikipiki na bajaji. Ila pia nawasihi waendesha bodaboda kufuata alama za barabarani, kuvaa kofia ngumu na kuvaa reflectors ili kuweza kujikinga na ajali wawapo barabarani” alizungumza mgeni rasmi Ofisa mnadhim wa Jeshi la Polisi Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Fortunas Musilimu.
  
Kuhusu Vilainishi vya Total
Total ni wasambazaji wa vilainishi mbalimbali vya magari, vyombo vya majini, mitambo na mashine za viwandani na za kilimo. Vilainishi hivi vimetengenezwa kwa ufanisi mkubwa ili kuwezesha injini ya chombo chako kuhimili hali ya hewa ya aina yoyote ile iwe joto au kipindi cha mvua kali. Vilainishi vya Total huimarisha, hulainisha, hupunguza msuguano na kuipa nguvu injini ya chombo husika kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi bila kuchoka wala kuchakaa.

0 comments:

Post a Comment