Monday, October 17, 2016


KAMPUNI ya simu za mkononi ya  Halotel Tanzania, leo inaadhimisha mwaka mmoja tangu ilipoanza kutoa huduma zake hapa nchini.
Kwa kipindi hicho cha mwaka mmoja, Halotel imeweza kufikia malengo yake kwa kiasi kikubwa ikiwamo kuongeza idadi ya watumiaji wa mtandao wake.
Kwa mujibu wa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hadi kufikia Septemba mwaka huu, ilikuwa na watumiaji wa mtandao huo wapatao milioni tatu na nusu.
Lakini pia, ripoti ya robo ya kwanza na ya pili ya mwaka huu ya TCRA inaonesha kuwa, Halotel imekua kwa kasi kwa upande wa ongezeko la wateja.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Tanzania, Lee Van Dai, alisema, mafanikio ya kampuni hiyo yametokana na ushirikiano uliopo kati ya wafanyakazi pamoja na ubunifu binafsi wa kibiashara wa kampuni hiyo.
Alisema kuwa, kwa sasa  Halotel ndio kampuni pekee inayotoa huduma bora za mawasiliano (IT) kwa kampuni kubwa  zikiwamo CRDB, NMB, BOA, FINCA, EXIM, SNV-Southern Netherlands na Development Organization.
Kwa mujibu wa Lee,  Halotel ina vifurushi mbalimbali kwa wateja wake kama vile Halo, Virushi vya wanafunzi, huduma maalumu kwa waajiri ya makundi mbalimbali kama vile waajiriwa serikalini, wanajeshi, askari polisi na walimu ambapo wanapata dakika 15 za mawasiliano bure kila siku.
“Lengo letu ni kuhakikisha kwamba tunawapiku washindani wetu katika soko na ndio maana huduma zetu zimekuwa zikipokewa vizuri sokoni. Tunajivunia kuwa kati ya kampuni bora katika utoaji wa huduma za mawasiliano nchini.
 “Kutokana na hali hiyo, tunaelekeza nguvu zetu zote katika kuboresha miundombinu yetu. Kwa mfano, hadi sasa tumekwisha jenga zaidi ya kilometa 20,000 za mkongo wa mawasiliano na zaidi ya vituo 2,700 kwaajili ya kupokea mawasiliano. Tumepeleka mitambo maalumu ya kuboresha mawasiliano katika vijiji 3,000 ambavyo awali havikuwa vimeunganishwa.
“Hiyo ni hatua ya kwanza ya kuhakikisha mawasiliano yanaenea nchini Tanzania,” alisema.
Alifafanua zaidi kuwa lengo la Halotel ni kuongeza idadi ya watumiaji kufikia milioni saba, ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017, na milioni tatu kwa watumiaji wa Halopesa.
Katika hatua nyingine, Naibu Mkurugenzi Mkuu huyo, alitumia fursa hiyo kuzindua huduma mpya ya Halopesa, huku akiwataka watanzania kujiunga na huduma hiyo, akidai kuwa imeenea sehemu kubwa nchini na ni ya haraka.
Ili kutumia huduma hiyo, mtumiaji anatakiwa kupiga  namba *150*88#, kisha kufuata maelekezo.
“Kwa kutumia Halopesa mteja anaweza kufanya malipo mbalimbali kama vile kutuma na kupokea fedha, kupokea au kutuma fedha kupitia benki na kulipia huduma nyingine kama Luku, Dawasco, and TV subscription-ZUKU, GEPF, TCU na Polisi,” alisema.
Halotel imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii. Hadai sasa kampuni imefanikiwa kutoa ajira za moja kwa moja zipatazo 25, 000 na 1,300 za moja kwa moja kwa watanzania.
Aidha kampuni inaboresha miundombinu ya kijamii kama vile utoaji wa huduma ya bure ya mtandao wa intaneti kwa shule 450, zenye umeme kwa miaka mitatu ijayo.
Kumekuwapo pia na ujenzi wa vyumba vya kopyuta kwa ajili ya huduma ya intaneti kwa kutumia modem katika Mikoa ya Pwani na Katavi.
Hivi karibuni Halotel imetoa shilingi miliioni 15 kwaajili ya kusaidia wananchi wa Kagera waliokubwa na tetemeko la ardhi.

0 comments:

Post a Comment