Tuesday, October 18, 2016


Waziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza na waandishi wa habari wakati wa sherehe fupi ya miaka kumi ya Metropolitan iliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Waziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza na wageni waalikwa wakati wa sherehe fupi ya miaka kumi ya Metropolitan iliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mkurugenzi Mtendaji wa Metropolitan Tanzania, Aman Mboma akizungumza na wandishi wa habari wakati wa sherehe fupi ya miaka kumi ya Metropolitan iliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla fupi ya miaka kumi ya Metropolitan wakimsikiliza Waziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage(hayupo pichani).

KAMPUNI ya Metropolitan Tanzania ilianzishwa kutokana na Kampuni ya Metropolitan International ambayo inamilikiwa na MMI Holdings.
Nchini Tanzania, Kampuni hii inayojihusisha na masuala ya Bima ilianza huduma zake rasmi Juni 7, 2016 ikiwa chini ya Kapuni ya Momentum Tanzania (PTY) Limited.

Leo hii Metropolitan Tanzania inaadhimisha miaka kumi yenye mafanikio katika utoaji wa huduma zake nchini, huku ikitangaza kuboresha huduma zake zaidi katika utoaji wa huduma za bima.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, katika hafla maalumu, Mkurugenzi Mtendaji wa Metropolitan Tanzania….. alisema kuwa miaka mitatu baada ya kuanzishwa kwa kapuni hiyo, walijikuta wakiwa katika orodha ya kampuni bora na zinazokua kwa haraka katika soko la bima nchini


“Tangu kupewa jina la Metropolitan Tanzania lililotokana na muungano wa Momentum and Metropolitan in 2013, kampuni hii imekuwa katika soko la bima nchini tangu wakati huo ikifanya vyema na ofisi zake zikiwa jijini Dar es Salaam,” alisema

Aliongeza kusema “Hivi karibuni kampuni ya MMI ikiwa kama mwekezaji wa kigeni nchini imewekeza jumla ya mtaji wa shilingi  za kitanzania bilioni 7.4. lakini kabla ya hapo Desemba 2105 mtaji wa kampuni hiyo ulikuwa shilingi za kitanzania bilioni 8.5”.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, jumla ya mtaji wa kampuni hiyo hadi sasa ni shilingi za kitanzania bilioni 16, hali ambayo inaifanya kampuni hiyo kuwa miongoni mwa kampuni zinazofanya vizuri katika soko la bima kwa kuwa na msimamo mzuri wa mtaji.

“Kampuni hii inapoadhimisha miaka kumi ya huduma zake nchini, niwafamishe wadau wetu wote kuwa tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora na kujiimarisha zaidi kibiashara ili tuendelee kuwapo katika soko kwa mafanikio”.

0 comments:

Post a Comment