Saturday, November 26, 2016Meneja Mauzo na Usambazaji Kinywaji cha Valeur kutoka Kampuni ya TDL, Mwesigwa Mchuruza(kushoto) akimkabidhi Hundi ya Shilingi Milioni mbili mshindi wa shindano la kuchekeza lililojulikana kama “Valeur Comedy Nights 2016”, Deogratias Mboya mara baada ya kutangazwa, shindano hilo lilifanyiaka mwishoni mwa wiki katika Bar ya Forty Forty Tabata jijini Dar es Salaam.Wapili kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Vuvuzela iliyokuwa ikiendesha shindano hilo, Evans Bukuku na Afisa Sanaa na Burudani kutoka Basata, Augustino Makame.Mshindi wa shindano la kuchekesha lililojulikana kama “Valeur Comedy Nights 2016”, Deogratias Mboya(katikati) akifurahi na kitita cha pesa taslimu Shilingi milioni mbili mara baada ya kukabidhiwa kama mshindi wa shidano hilo 2016 lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Bar ya Forty Forty Tabata jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Afisa Sanaa na Burudani kutoka Basata, Augustino Makame, Meneja Mauzo na Usambazaji Kinywaji cha Valeur kutoka Kampuni ya TDL, Mwesigwa Mchuruza na Mchuruza na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Vuvuzela iliyokuwa ikiendesha shindano hilo, Evans Bukuku.


Deogratius Mboya bingwa wa kuchesha Dar.
Na Mwandishi Wetu.
Deogratius Mboya amejinyakulia ubingwa wa kuchekesha katika shindano lililomalizika mwishoni mwa wiki chini ya udhamini wa kinywaji cha Valeur lililojulikana kama ‘Valeur Comedy Nights 2016” na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi milioni mbili(2,000 000/-),Tuzo maalum ya ushindi na mafunzo kwa videndo na kampuni ya Vuvuzela kwa muda wa miezi sita.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Hamphley Richard ambaye alizawadiwa Tuzo maalumu ya mshindi wa pili pamoja na mafunzo kwa videndo na kampuni ya Vuvuzela kwa muda wa miezi sita na nafasi ya tatu ni Adam Mbweche ambaye pia alizawadiwa tuzo maalum ya ushindi wa nafasi ya tatu pamoja na mafunzo kwa videndo na kampuni ya Vuvuzela kwa muda wa miezi sita.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mgeni raasmi Afisa Sanaa na Burudani kutoka Basata, Augustino Makame aliwapongeza Kampuni ya Vuvuzela kwa kuendesha shindano hilo katika kiwango cha hali ya juu lakini pia kwa hamasa ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliohudhuria shindano hilo hii inaonyesha dhahili watu wanaelewa sasa Sanaa ya uchekeshaji.
Makame alimaliza kwa kutoa wito kwa Kampuni ya Vuvuzela kutanua uwigo sasa wa kufikira kwenda kisaka vipaji pia na mikoani.
Nae Meneja Mauzo na Usambazaji Kinywaji cha Valeur kutoka Kampuni ya TDL, Mwesigwa Mchuruza alimpongeza mshindi kwa kujinyakulia kitita cha Shilingi Milioni mbili na kumuomba akaitumie vizuri kwani ni pesa ndogo kwa starehe lakini ni pesa nyingi sana kama akiifanya kama mtaji wa ujasiliamali unaweza kumtoa hapo alipo.
Mchuruza aliwapongeza pia washiriki wote kwa kufika hatua ya fainali lakini mwisho wa siku lazima apatikane mshindi mmoja lakini pia aliwapongeza kwa kuja na mashabiki wao kwani wamelifanya shindano kuwa lenye hamasa ya hali ya juu ukilinganisha na mwaka jana.
Washiriki waliofanikiwa kuingia fainali walikuwa kumi na nane(18) kutoka vitongoji mbalimbali vya Mkoa wa Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment