Tuesday, January 17, 2017

  Katibu msaidizi wa Balozi  wa India nchini(Second Secretary of High Commission of India), Amalendu Mahapatri (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa madarasa mawili ya darasa la saba katika Shule ya Msingi Zanaki kwa msaada wa jumuia ya Kihindi ya Kalamandalam waishio nchini Tanzania.Jumuia hiyo ilitoa msaada wa Ukarabati wa madarasa mawili,Vyoo,Mbao za kufundishia,Makabati,enka za mabegi na ununuzi wamadawadi.Kulia ni Mwanachama wa taasisi hiyo na Meneja Mlimani City, Gilish Kumar na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sam Idicula.

  Katibu msaidizi wa Balozi  wa India nchini(Second Secretary of High Commission of India), Amalendu Mahapatri (kulia) akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Zanaki, Radhia Mfalingundi madawadi  na ukarabati wa madarasa na vyoo ikiwa ni msaada uliotolewa na taasisi ya Kihindi ya Kalamandalam nchini Tanzania.Makabidhiano hayo yalifanyika Dar es Salaam leo.

  Baadhi ya wanafunzi wakiweka mabegi yao ya madaftari katika enka maalumu zilizotolewa na taasisi ya Kihindi ya Kalamandalam nchini Tanzania .


Picha ya Pamoja mara baada ya makabidhiano.

0 comments:

Post a Comment