Tuesday, January 17, 2017

Meneja Mkuu wa Mlimani City, Pastory Mroso,((katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi maalum wa promosheni ya “Fanya shomping Mlimani City ushinde Gari” katika kipindi cha msimu wa sikukuu ya Chrismass na Mwaka Mpya.Kulia ni mwakilishi kutoka Gaming board, Abdalah Singano.Wengine ni wafanyakazi wa Mlimani City.
 
 
Katika kusherehekea Sikukuu za X-Mas na Mwaka Mpya, uongozi wa Mlimani City kwa kushirikiana na wafanyabiashara wenhye maduka ndfani yake umetangaza ofa maalumu kwa wateja  wake wanataofanya manunuzi katika msimu huu wa sikukuu.
Ofa hiyo inatoa fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwamo gari jipya kabisa la kisasa aina ya Renault Kwid, lenye thamani ya Dola za Marekani 8,500. 
Zawadi nyingine ni Vocha za Manunuzi kwa washindi 10, zenye thamani ya 100,000/- kila mmoja, ambao watapatikana kwenye droo zitakazokuwa zikifanyika kila wiki.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja mkuu wa Mlimani City Ndugu Pastory Mrosso wa kila alisema kuwa washindi wa kila wiki watafanya manunuzi katika duka lolote ndani ya Mlimani City kwa kutumia vocha zao.
Promosheni hii maalumu imeanza Desemba 15 na inatarajia kufikia mwisho Januari 7, 2017, ambapo droo ya kubwa ya kupata mshindi wa gari itafanyika wiki ya pili ya Januari 2017.
Meneja huyo aliwaomba watanzania kuendelea kufanya manunuzi yao katika maduka ya Mlimani City, kutokana na kuwajali wateja wake na kutoa huduma zinazokwenda na wakati na hasa katika kipindi hiki cha X-Mas na Mwaka Mpya
 
 
 
 

0 comments:

Post a Comment